Lyrics | Diamond Platnumz - Acha Nikae Kimya.| Official Lyrics

                                       
                                                
Nasema walau nina kidogo na mashabiki wananiambia mbona hausemi chochote
Ah, si uko nao siku zote ama ulezi unafanya uogope
Ah na media pande zote wanalalama kiongozi atoke
Ah nchi inaingia matope niende wapi na mimi mtoto wa wote,
Yaani lawama, acha nikae kimya, niongee, kimya (ooh ninyamaze mimi)
Nikae kimya nisemee (kimya) mama kaniambia (acha nikae kimya)
Ooh nifunge m[u]domo, mimi bado m[u]dogo nisiseme (kimya)

Verse

Ni mengi majaribu najaribu kuepuka yasije nicost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alipokamatwa iliniumiza sana mitandaoni kila kona
Uongo na ukweli unashonwa kila nyumba inanong’ona, ahh, ooh Tanzania
Mara kibembe Dodoma wabunge pinzani wamegoma juzi akapotea na Roma
Ohh Tanzania
Najaribu kunyamaza Makame hataki ohh ananiambia walau nina kidogo
Nyumbani nafungwa geti niende kwa Mangi kununua super gate
Napewa za chini ya kapeti kuna redio imevamiliwa eti
Ehh, napita kwenye magazeti nakuta lundo la watu wameketi
Ehh badala ya kutafuta senti wanabishana tu mambo ya vyeti

Acha nikae kimya (nisiongee ) nikae kimya (ninyamaze kabisa)
Nikae kimya (ulimi koma) kimya (usije kuniponza) acha nikae kimya
(nifunge bakuli langu) nikae kimya (nikojoe nikalale) kimya
Mimi bado mdogo sana mama kanimbia

Bridge

Najiuliza wapi (wapi) najiuliza wapiii, tunakwenda wapi
Wapi, kila siku maneno, wapii, hatuwajengi jamaa
Mimi na wewe ni taifa moja, Kambarage baba mmoja
Sasa tofauti za nini tushikamane tukaijenge Tanzania

Comments

Popular posts from this blog

Lyrics | Harmonize - Niambie.| Official Lyrics

Lyrics | Diamond Platnumz - Mapenzi Basi.| Official Lyrics

Lyrics | Diamond Platnumz - Lala Salama.| Official Lyrics